(ABNA24.com) Rais Hassan Rouhani ambaye leo alikuwa akizungumza katika kikao cha baraza la mawaziri mjini Tehran, ameashiria madai ya maafisa wa serikali ya Marekani kwamba Washington iko tayari kuisaidia Iran kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona na kusema: Vikwazo vya kidhalimu, haramu na vya kigaidi vilivyowekwa na Marekani dhidi ya taifa la Iran vimesababisha matatizo mengi kwa wananchi wa Iran.
Rais Rouhani ameongeza kuwa: Kama kweli Wamarekani wanataka kuisaidia Iran basi wanapaswa kuketi kando na kuacha kuzuia shughuli za Wairani katika nyanja mbalimbali kama uuzaji wa mafuta, mabadilishano ya kibenki, ununuzi wa dawa na hata malighafi.
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza pia kwamba, Marekani ndiye mhusika mkuu wa jinai kubwa zaidi za kigaidi katika eneo la magharibi mwa Asia na nchini Iran na kuongeza kuwa, fikra za Wamarekani na misingi ya fikra zao za kigaidi na zisizo sahihi imedhihirika zaidi kwa walimwengu katika kipindi cha sasa.
Rais Rouhani amesema kuwa Wairani watavuka kipindi kigumu cha sasa kwa ushirikiano, muawana na umoja wao na kuongeza kuwa, ulimwengu ni mdaiwa wa utamaduni wa Uislamu na Iran katika masuala mengi ya kisayansi na kiafya.
Vilevile ameashiria hatua ya Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei ya kuupa mwaka huu mpya wa 1399 jina la Mwaka wa Ustawi Mkubwa katika Uzalishaji na kusema, ili kufikia lengo hilo kuna udharura wa kuwa na uhusiano mzuri na nchi mbalimbali duniani hususan nchi jirani.
...........
340